CLATUS CHAMA AAMUA KUONDOKA SIMBA KUTAFUTA CHANGAMOTO SEHEMU NYINGINE
Taarifa za uhakika zilizotufikia kutoka klabu ya Simba zinasema kuwa mpango wa kumshawishi kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Cletus Chama kusaini mkataba mpya zimegonga mwamba baada ya mchezaji huyo kuwaelekeza kuwa ameamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapofikia tamati. Mchezaji huyo amekuwa kwenye kiwango bora sana tangu ilipotangazwa kuwa amesamehewa kutoka kufungiwa Kwa makosa ya utovu wa nidhamu ambayo hayakuwekwa wazi hivyo alisimamishwa na kupelekwa kamati na nidhamu ya klabu hiyo japo alisamehewa bila kufika mbele ya kamati hiyo. Inasemekana kambi ya mchezaji huyo imechukizwa na shutuma mbalimbali ambazo amekuwa akipewa mteja wao huyu Kila mara mambo yanapoonekana kwenda kombo hasa timu hiyo ikifanya vibaya katika mechi mbalimbali. Mchezaji huyo amekuwa akishutumiwa kucheza chini ya kiwango hasa katika mechi kubwa zikiwemo mechi dhidi ya mtani wao Yanga. Kambi ya mchezaji huyo pia inaona mteja wao hapewi heshima inayostahili Kwa amekuwa mchezaji ambaye h...