CLATUS CHAMA AAMUA KUONDOKA SIMBA KUTAFUTA CHANGAMOTO SEHEMU NYINGINE

 


Taarifa za uhakika zilizotufikia kutoka klabu ya Simba zinasema kuwa mpango wa kumshawishi kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Cletus Chama kusaini mkataba mpya zimegonga mwamba baada ya mchezaji huyo kuwaelekeza kuwa ameamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapofikia tamati.


Mchezaji huyo amekuwa kwenye kiwango bora sana tangu ilipotangazwa kuwa amesamehewa kutoka kufungiwa Kwa makosa ya utovu wa nidhamu ambayo hayakuwekwa wazi hivyo alisimamishwa na kupelekwa kamati na nidhamu ya klabu hiyo japo alisamehewa bila kufika mbele ya kamati hiyo.


Inasemekana kambi ya mchezaji huyo imechukizwa na shutuma mbalimbali ambazo amekuwa akipewa mteja wao huyu Kila mara mambo yanapoonekana kwenda kombo hasa timu hiyo ikifanya vibaya katika mechi mbalimbali. Mchezaji huyo amekuwa akishutumiwa kucheza chini ya kiwango hasa katika mechi kubwa zikiwemo mechi dhidi ya mtani wao Yanga.


Kambi ya mchezaji huyo pia inaona mteja wao hapewi heshima inayostahili Kwa amekuwa mchezaji ambaye huibeba timu hiyo katika mechi mbalimbali na za michuano mbalimbali kama vile ligi ya Mabingwa Afrika na kombe la shirikisho barani Afrika.


Kiwango ambacho mchezaji huyo amekuwa akikionesha siku za karibuni katika ligi kuu NBC Tanzania na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kama anafanya uchonganishi Kwa mashabiki na viongozi wao kuelekea mwisho wa mkataba wake.


Hivyo ni swala lisilofichika kuwa mchezaji huyo na kambi yake inayomsimamia wameamua Kwa pamoja kuwa mchezaji huyo hatoongeza mkataba mpya na ataondoka akiwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.


Je mchezaji huyo ataelekea wapi? Endelea kuwa nasi katika ukurasa huu 💪

Comments

Popular posts from this blog

BREAKING! Wydad Casablanca are officially out of the Champions League (GS)

ALWAYS A South African FOOTBALL LEGEND Mkhonza